Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Baqir Darwish, mkuu wa utoaji taarifa wa Jumuiya ya Haki za Binadamu ya Bahrain, katika mkutano na waandishi wa habari wenye anuani ya uwekaji kumbukumbu ya mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu na ukiukaji wa sheria za kimataifa wakati wa “vita vya kulazimishwa vya Marekani na Israel dhidi ya Iran” uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli Parsia mjini Qum Iran, alisema: utawala wa Bahrain katika ngazi mbalimbali unakiuka haki za binadamu dhidi ya Mashia na bado unaendelea na ukiukaji huu dhidi ya watu wengine wa nchi hii.
Aliongeza kuwa: tangu mwaka 2011 hadi sasa, zaidi ya watu elfu ishirini nchini Bahrain, ambao wengi wao walikuwa Mashia, wamekamatwa kwa sababu tu ya kutoa maoni yao na kutumia uhuru wa kujieleza. Bila shaka baadhi pia walikuwa watu wa Kisunni ambao walifungwa jela. Aidha katika kipindi hiki maelfu ya watu wamepitia mateso ya kikatili, na mamia ya hukumu za vifungo virefu zimetolewa dhidi yao.
Utawala dhalimu wa Bahrain haumruhusu mtu yeyote uhuru wa kujieleza
Mwanaharakati huyu wa haki za binadamu aliendelea kusema: utawala wa Bahrain hata watu wa kawaida ambao walitoa salamu za rambirambi kutokana na shahada ya Imam Khamenei (ra) au waliosimamisha bendera nyeusi pia walikandamiza kwa nguvu, walikamatwa na kufungwa jela. Watu hawa walihukumiwa kwa adhabu hizi kwa sababu tu ya kuonesha imani yao.
Darwish aliendelea kusema: utawala huu dhalimu haumruhusu mtu yeyote uhuru wa kujieleza, na kila mtu anaekosoa, hata kwa kiwango cha ujumbe mfupi wa mtandao (tweet), hutiwa jela na kuteswa. Katika muktadha huu kuna mamia ya wafungwa ambao wamepoteza maisha yao chini ya mateso.
Vita dhidi ya Iran ni mfano wazi wa ukiukaji mkubwa wa kanuni za Mikataba ya Geneva na ni miongoni mwa uhalifu wa kivita wa kimataifa
Mwanaharakati huyu wa kisiasa, huku akirejelea vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema: kuwalenga raia, wakiwemo watoto na wanafunzi, na kuharibu miundombinu isiyo ya kijeshi kama vile nyumba za makazi, vituo vya matibabu na maeneo ya kitamaduni, ni mfano wazi wa ukiukaji mkubwa wa kanuni za Mikataba ya Geneva na ni miongoni mwa uhalifu wa kivita wa kimataifa unaohitaji uwajibikaji na adhabu. Miongoni mwa uhalifu huu ni shambulio dhidi ya shule ya watoto huko Minab ambapo zaidi ya wanafunzi mia moja wa kike na kiume walipata shahada.
Aliongeza kuwa: Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, kutokana na uwepo wake usio halali, kinakabiliwa na upinzani wa maoni ya umma, na watu wa Bahrain wanataka kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini mwao.
Watawala wa nchi za Kiarabu wanawakamata raia wa Kishia katika nchi hizi kwa visingizio visivyo na msingi
Katika mwendelezo wa mkutano huu, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Abbas Shubbar alisema: watawala wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Bahrain na Kuwait wanawakamata raia wa Kishia katika nchi hizi kwa visingizio visivyo na msingi.
Aliongeza kuwa: katika siku na wiki zilizopita, watu wengi wa kidini, wa hawza na wa vyuo vikuu miongoni mwa raia wa Kishia katika nchi kadhaa za Ghuba ya Uajemi, zikiwemo UAE, Kuwait, Saudi Arabia na Bahrain, kutokana na vita vya eneo hili, wameitwa, wamehojiwa na kukamatwa; bila hata kuwepo kwa mashtaka maalum dhidi yao.
Mwanazuoni huyu wa Kishia aliendelea kusema: idara ya usalama ya serikali ya UAE, katika hatua ya kuipinga Iran, imewakamata baadhi ya raia wa Kishia katika nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusishwa na “Wilayat al-Faqih” na kwa visingizio visivyo na msingi vya kuhusika katika “shughuli za siri” kwa lengo la kudhoofisha umoja wa kitaifa na kuleta hali ya kukosekana kwa utulivu nchini kupitia kupanga operesheni za “uhujumu wa kimfumo” ndani ya mipaka yake.
Zaidi ya wafungwa wa kisiasa 5000 wapo katika magereza ya Bahrain
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shubbar alibainisha: kukamatwa huku kumefanyika katika hali ambayo wakati wa uvamizi wa Marekani na Wazayuni dhidi ya Iran, UAE imepiga marufuku uchapishaji wa picha na video zozote za mashambulizi ya Iran dhidi ya maslahi ya Marekani katika nchi hiyo, na pia imewakamata watu waliofanya hivyo.
Aliongeza kuwa: Aal Khalifa katika muongo uliopita, mbali na kuwaua maelfu ya Mashia, pia wamewakamata wapinzani wa kisiasa na viongozi wao, kuwafunga jela na kuwanyang’anya uraia wao. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, zaidi ya wafungwa wa kisiasa 5000 wapo katika magereza ya Bahrain, ambapo baadhi yao wamehukumiwa kifungo cha maisha na hata adhabu ya kifo kwa visingizio visivyo na msingi.
Aal Khalifa baada ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni mwezi Septemba 2020, waliongeza vikwazo zaidi dhidi ya Mashia
Mwanaharakati huyu wa haki za binadamu alisema: Aal Khalifa baada ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni mwezi Septemba 2020, walibana zaidi harakati za Mashia ili kukandamiza sauti yoyote ya upinzani dhidi ya uhalifu wa Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Aliongeza: sasa pia, baada ya uvamizi wa adui wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran, Mashia wa Bahrain wamesimama upande sahihi wa historia na, kinyume na utawala wa Aal Khalifa, wanaiunga mkono Iran; watawala dhalimu kwa kuunda hali ya hofu na vitisho kote nchini wanajaribu kuzima mapema maandamano yoyote ya kuiunga mkono Iran.
Maoni yako